Jumamosi, 17 Desemba 2016

Serikali imewataka wakuu wa mikoa, wilaya na mamlaka ya serikali za mitaa

Serikali imewataka wakuu wa mikoa, wilaya na
mamlaka ya serikali za mitaa na miji kuweka
utaratibu na mfumo utakaowasaidia wafanya
biashara wadogo wadogo (wamachinga) kufanya
biashara zao kwa kuzingatia utaratibu mzuri ili
kuwawezesha kujipatia kipato cha kuendesha
maisha yao na familia zao.


Wito huo umetolewa mjini Dodoma na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene na
kusisitiza kuwa wamachinga wana haki ya
kufanya kazi zao kwa utaratibu mzuri na
mamlaka za serikali zinapaswa zitambuwe
mchango wao katika uchumi.


“Lazima wajipange kutekeleza maagizo ya
mheshimiwa rais kwa ufasaha,weledi na umakini
mkubwa ili kuwasaidia ndugu zetu wamachinga
kufanya biashara zao kujipatia kipato cha
kuendesha maisha yao na familia zao na waagia
wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na mamlaka
za serikali za mitaa kuhakikisha zinatekeleza
agizo la mheshimiwa rais na sio kususia na
kuwaacha wamachinga wafanye biashara zao
kiholela,” alisema Simba
chawene.
BY: EMMY MWAIPOPO

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni